Mchezo
wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya
jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio
cha chini kitakua ni silingi elfu saba..
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangaza viingilio vya mchezo huo
ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni, kuwa ni tsh
7,000 kwa majukaa yenye rangi ya kijani, bluu na rangi ya chingwa, VIP B
& C tsh 20,000 na VIP A tsh 30,000.
Tiketi
za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo jumamosi asubuhi saa 2
kamili katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Mchezo
huo wa Ngao ya Jamii utachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo,
(Dsm), akisaidiwa na Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Josephat Daud Bulali
(Tanga), mwamuzi wa akiba Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa
mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni