FOWADI
wa Barcelona Pedro sasa atahamia Chelsea baada ya Klabu hiyo kukubali
kulipa Pauni Milioni 22 kwa mkupuo kitu ambacho Manchester United
waligomea kulipa.
Kwa
muda mrefu iliaminika kuwa Pedro atatua Old Trafford huku kukiripotiwa
kuwa tayari ameshaafikiana maslahi yake binafsi lakini kusita kwa Man
United kulipa kwa mkupuo mmoja Dau ambalo Barca walikuwa wakitaka
kumetoa mwanya kwa Chelsea kutumbukia na kukubali kulipa Dau hilo lote
na kumnasa Staa huyo.
Man
United walikuwa tayari kulipa Dau la Pauni Milioni 17.7 mbele na kisha
kulipa pole pole Pauni Milioni 3.6 zikiwa nyongeza ambazo zitaendana na
mafanikio atakayopata Mchezaji huyo akiwa na Man United.
Kitu hicho Barca waligomea na kutaka Fedha zote kwa mkupuo na hapo ndipo Chelsea wakawapiku Man United.
Inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa Pedro, mwenye Miaka 28, atapimwa Afya yake huko Stamford Bridge na kisha kusaini Mkataba.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni