LOGO

IMG_0557-0.JPG
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupigwa.
Mechi ya mapema itawakutanisha KMKM dhidi ya Mtende kuanzia majira ya saa 9:00 alasiri.
Mechi ya pili itaanza majira ya saa 11:00 jioni ambapo mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc watashuka dimbani kuoneshana kazi na mabingwa watetezi wa kombe hilo, KCC ya Uganda.
Hii itakuwa mechi kali kutokana na upinzani wa timu hizi mbili na ikizingatiwa juzi juzi zilikutana nchini Uganda katika mechi ya kirafiki ambapo Azam fc ilitandikwa mabao 3-2.
Usiku majira ya 2:00, Yanga itashuka dimbani kuchuana na Taifa ya Jang’ombe.
Kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm pamoja na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa jana walikuwepo uwanja wa Amaan Zanzibar kushuhudia mahasimu wake Simba wakichuana vikali na vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, Mtibwa Sugar FC.

Katika mchezo huo bao pekee la Henry Joseph Shindika lilitosha kuwaliza Simba 1-0.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top