Ratiba ya ligi kuu ya Vodacom
Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi
hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti
nchini na kumalizika Mei 7, 2016.
TFF inavisisitiza vilabu
kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa
dirisha hilo la usjaili kesho siku ya Alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya
kufungwa kwa usajili huo hakutakuwa na muda tena wa nyongeza.
Kwa klabu ambayo haitawasilisha
malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili (U$D 2000)
mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo
yatakapofanyika.
Michezo saba itachezwa siku ya
ufunguzi Jumamosi Septemba 12 katika viwanja tofauti ambapo mechi
zitakuwa kama ifuatavyao; Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda –
Mtwara), African Sports Vs Simba SC (Mkwakwani – Tanga), Majimaji Vs JKT
Ruvu (Majimaji – Songea), Azam FC Vs Tanzania Prisons (Azam Complex –
Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar (Kambarage – Shinyanga), Toto
Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba – Mwanza), na siku ya jumapili Young
Africans Vs Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).
Ratiba kamili hii hapa, angalia mechi zote za timu yako hapo chini…
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni