LOGO


 
Kocha mpya wa Simba SC Goran Kopunovic ameanza vyema kibarua chake baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa kwanza kuiongoza Simba SC toka aanze kazi hapo jana.
Katika mchezo huo wa kombe la mapinduzi wa kundi C ulioanza majira ya saa kumi na moja jioni ulishuhudia Simba SC ikingoja mpaka dakika ya 54 kuandika goli pekee la ushindi kupitia kwa Said Ndemla.
Katika kipindi cha kwanza kilikuwa cha kufiziana kwa pande zote mbili huku mpira ukichezwa zaidi katika eneo la kati ya uwanja na kukikosekana mbinu za kupenya katika kila ngome, kitendo kilichopelekea kutokuwepo kwa nafasi ya wazi katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili mambo yalikuwa tofauti huku kasi ya mchezo ikiongezeka tofauti na kipindi cha kwanza na kila timu ikionesha nia ya kupata goli la kuongoza na ndipo shuti la mita 22 la Said Ndemla lilitosha kuwatoa kifua mbele Simba SC katika mchezo huo.
Kwa matokeo hayo msimamo wa kundi hilo la C unabaki kama ulivyo kuwa likiwa linaongozwa na JKU yenye point 4 sawa na Mtibwa sugar tofauti ikiwa katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa, huku Simba SC ikishika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 3 na Mafunzo wakiwa wa mwisho bila na pointi yoyote.
Michezo ya mwisho ya kundi C itachezwa januari 5 mwaka huu ambapo Simba SC watakabiliana na na JKU huku Mtibwa Sugar wakichuana na Mafunzo.
Kesho kutakuwa na michezo ya pili kwa kundi A na B ambapo Azam FC watakabiliana KMKM saa kumi na moja na saa tisa KCCA wakikabiliana na Mtende, wakati Yanga wakicheza na Polisi saa mbili usiku wakati Taifa Jang'ombe wakicheza na Shaba katika uwanja wa mao Tsung.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top