Kipa aliyewahi kudakia Moro united, Simba SC na timu ya taifa Juma Kaseja ameondolewa kwenye usajili wa yanga katika michuano ya kombe la shirikisho ambalo yanga itafungua na timu ya jeshi la Botswana.
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Mulo ametabainisha kuwa yanga wametuma majina 24 ya wachezaji kwenda CAF, ambayo ndiyo yatakayo ruhusiwa kucheza kwenye michuano ya kombe la shirikisho mwaka huu.
Mulo alisema kuwa Kaseja hajaambatana na timu kwenda Zanzibar na jina lake halipo katika usajili wa yanga katika michuano ya kombe la shirikisho, kutokana na Kaseja kutofanya mazoezi na wenzake kwa muda sasa.
Akizungumzia kuhusu suala la mkataba wa Kaseja, ambalo mwakilishi wa Kaseja mara kadhaa amenukuliwa akisema yanga wamekeuka mkataba wa Kaseja na hivyo mkataba baina ya Kaseja na yanga umeshavunjika.
Mulo alisema suala hilo limeshafika katika dawati la kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya yanga na wanangoja ufafanuzi toka katika kamati hiyo inashughulikia masuala yote ya mkataba na sheria ndani ya yanga.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni