Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA
limeahidi kutoa dola laki Saba na nusu kwa shirikisho la soka la
Tanzania kwaajili ya maandalizi ya Timu ya Taifa Tanzania kuelekea kombe
la Dunia mwaka 2018.
Shirikisho la soka la Tanzania (TFF)
limepokea Taarifa kutoka Fifa ya kupatiwa fedha kwa ajili ya Maandalizi
ya Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ( Taifa stars ) ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2018.Kwa upande wake Rais wa shirikisho hilo Jamal malinzi Amethibitisha Taarifa hiyo kuwa FIFA Imeahidi kuwapatia fedha kwaajili ya kufanya maandalizi ya Timu ya Taifa kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia .
Malinzi amesema kiasi hicho cha fedha pia watakitumia kuanzisha miradi mbalimbali ili kuliwezesha shirikisho kuwa na fedha za kutosha na kuendeleza shughuli za kimichezo kwa upande wa soka.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni