Mchezaji wa Cameroon West Ham Alex
Song amestaafu kucheza soka ya kimataifa baada ya kutopata mwaliko wa
kikosi cha timu ya taifa kitakacholiwakilisha taifa hilo katika kombe la
nchi za Afrika.
Song mwenye umri wa 27, ambaye kwa sasa anachezea
timu ya ligi kuu ya Uingereza West Ham kupitia mkopo wa Barcelona sasa
ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za
mwisho na Cameroon kuvunjika.Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni