WAKATI Simba ikimsajili straika wa Gor Mahia ya
Kenya, Mganda Dan Sserunkuma ambaye amechukuwa nafasi ya Mkenya Raphael
Kiongera, Yanga nayo itajibu mapigo kwa kusajili straika matata kutoka
Liberia anayekipiga Malaysia, lakini inafanya siri sana.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa straika
huyo anayetarajia kutua nchini wakati wowote ili kumwaga wino, anaweza
kuchukuwa nafasi kati ya Hamis Kiiza ambaye kiwango chake
hakijaliridhisha benchi la ufundi licha ya kwamba ana mkataba wa zaidi
ya miezi sita na Yanga.
Kwa mujibu wa kanuni, ili kumpisha Mliberia huyo,
Yanga itapaswa kusitisha mkataba na mchezaji mwingine aliyeko kwenye
usajili wao na pande zote mbili zikubaliane, lakini kinyume na hapo
Yanga hairuhusiwa kusajili.
Habari za ndani zinadai kwamba benchi la ufundi
limeuambia uongozi kwamba Kiiza hana manufaa kwa sasa na hata morali
yake ipo chini hivyo kuendelea kubaki naye ni kufuja fedha ambazo
zingesajili mashine nyingine ya maana.
Lakini mmoja wa marafiki wa Kiiza aliiambia
Mwanaspoti mazoezini jana Ijumaa kwamba mchezaji huyo anaelewa kila
kinachoendelea ndio maana ameamua kukaa tayari kwa lolote ingawa
viongozi wa usajili wamemzuga kwamba atulize mzuka haachwi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati ya
usajili, zinasema kwamba Maximo ameridhia mchezaji huyo asajiliwe kwa
maelezo kwamba kiwango chake kiko juu ya Kiiza, lakini Mliberia huyo
ambaye jina lake wanafanya siri ameiambia Yanga kwamba anataka mkataba
wa mwaka mmoja na si miwili kama klabu hiyo inavyong’ang’ania.
Kwa mujibu wa viongozi mchezaji huyo amecheza misimu miwili kwenye Ligi ya Malaysia.
Usajili wa Mliberia huyo umepiga chini ujio wa
straika mwingine Mzambia ambaye Maximo aliangalia maelezo yake na
kuwaambia viongozi kwamba ni wa kawaida sana.
Tayari Yanga imemsajili kiungo Mbrazil Emerson de
Oliviera Roque lakini wamedai kuhakikisha wanapata straika matata
atakayeiwezesha Yanga kupata mabao katika mechi zao za Ligi Kuu na
michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani.
Emerson amechukuwa nafasi ya Geilson Santos ‘Jaja’
ambaye ameshindwa kurudi nchini alipokwenda kwao kwenye mapumziko
mafupi baada ya ligi kusimama.
Hivi karibuni kulikuwepo pia taarifa za kumnasa
kiraka kutoka Zambia, Jonas Sakuwaha anayekipiga TP Mazembe ambaye
ilidaiwa kuamua kuachana na timu hiyo ili kwenda kujaribu changamoto
mpya pamoja na straika wa AS Vital ya Uganda, Yunus Sentamu. Kwa sasa
Yanga inajiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba ya Desemba
13.
MWANASPOTI
MWANASPOTI
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.