Uongozi wa Yanga umeingia mchecheto kwa kuanza kuwakataa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kujadili suala lao na mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Habari za ndani zinasema kuwa Yanga imeandika barua hiyo TFF ikidai kuwa haina imani
na Zakaria Hans Pope na Iman Madega ambao ni wajumbe kwenye kamati hiyo.
Chanzo hicho kimesema kuwa Yanga
wamedai kuwa hawana imani na wajumbe hao kwa vile Hans Pope ana husika moja kwa
moja kwenye suala hilo wakati Madega kuna tofauti baina yao.
“Unajua hata ile kupeleka muhtasari
wa mkutano wa marekebisho ya katiba ya Yanga walichelewa kupeleka kwa sababu
hiyo hiyo walijua tu kwa watu hao lazima ingekwama,”kilisema chanzo hicho.
Iman Madega
Chanzo hicho kilisema kuwa Kamati
hiyo itakutana wiki ijayo Septemba 8 ambapo mbali na suala hilo la Okwi pia
watapitia mapingamizi ya usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu na muhtasari wa
katiba ya Yanga.
Katibu Mkuu wa TFF, Celestine
Mwesigwa alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema,”Nipo nje ya ofisi kwa
sasa, sipo tayari kuzungumzia suala hilo, mtafute Mkurugenzi wa Mashindano wa
TFF, Boniface Wambura.”
Wambura alipotafutwa alisema,”Siwezi kuzungumzia suala hilo, nipo kwenye kikao.”
Ofisa habari wa Yanga, Baraka
Kizuguto alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema,”Sina taarifa hizo.”
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni