LOGO

Timu ya Soka ya Coastal Union ya Tanga inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara imeibuka na ushindi wa magoli 10-0 dhidi ya Timu ya Falcon FC ya Visiwani Pemba katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani Visiwani Pemba
Alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Coastal Union aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya, Itubu Imbem raia wa Kongo,aliefungia Coastal Union magoli matatu pekeake HAT TRICK katika mechi yao kirafiki dhidi ya Falcon FC ya Pemba
Falcon FC, iliyowahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, inashiriki Ligi Daraja la Kwanza visiwani humo baada ya kuteremka daraja na juzi ilikumbwa na dhahama hiyo ya mabao kutoka kwa mabingwa wa Tanzania Bara 1988 waliosajili wachezaji wengi wapya baada ya kikosi chao kufanya vibaya msimu uliopita huku kukitokea mgogoro wa kiuongozi.

Coastal Union walioonekana kujiamini na kujipanga vilivyo, walilishambulia kwa fujo lango la Falcon na kupata magoli hayo, wakipata magoli matano katika kila kipindi.

Magoli ya mengine Coastal Union yalifungwa na Abasi Athumani ambaye alipachika matatu pia (Hat-Trick) wakati Mahundi Petro na Mbwana Hamisi kila mmoja akipachika goli moja.
Mchezaji mwingine aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia, Mkenya Rama Salim naye  alitikisa nyavu mara mbili na kuhitimisha karamu ya magoli kwa Coastal inayonolewa na Yusuph
Chippo alisema kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya wakiwa visiwani humo wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza Septemba 20 mwaka huu.
“Sasa kikosi changu kimeimarika kwani juzi tuliifunga Opec ya kisiwani hapa mabao 11-0, hivyo kikosi changu kipo tayari kushiriki Ligi Kuu tukianzia na mechi yetu dhidi ya Simba kwa kuchukua pointi tatu muhimu," alisema Chippo baada ya mechi hiyo.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top