LOGO

Shirikisho la Mpira wa miguu Africa CAF limeifungia nchi ya BENIN kwa miaka miwili kucheza mashindano yote ya vijana baada ya kutumia wachezaji wanne waliovuka umri kwenye mechi ya kuwania kufuzu Fainali za mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Afrika mwakani nchini Niger dhidi ya Mali.
Wachezaji hao ni Ibilola Aron aliyezaliwa Desemba 10 mwaka 1997, Ogoubiyi Oluwa aliyealiwa Oktoba 26, 1997, Oreko Evode aliyezaliwa Desemba 24, 1997 na Amoussou Tony aliyezaliwa Septemba 19, 1997.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Taarifa zilizotumwa CAF Septemba 2 mwaka 2013 zimesema wachezaji hao walizaliwa Januari 1 mwaka 1998 na wako huru kucheza mashindano hayo.
Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya U-17 Afrika baada ya kupitia kanuni ya 33 ya ibara ya 11 imeamua kuiondoa Benin, na Mali kusonga mbele ambayo sasa itamenyana na Tunisia katika hatua ya mwisho wa mchujo.
Pia Kamati hiyo imelitia hatiani Shirikisho la Soka la Benin kwa kudanganya umri wa wachezaji hao katika taarifa zao walizotuma CAF na kwa kutumia Ibara ya 37 ya kanuni za mashindano hayo, inayosema: “Makosa coyote ya kiuongozi juu ya usajili wa wachezaji au kudanganya tarehe za kuzaliwa, chana husika kitafungiwa kwa miaka miwili kwenye mashindano yote ya vijana ya CAF,”.
Hiyo inamaansha kwamba, Benin imefungiwa kushiriki mashindano ya U-17, U-20 na U-23 kwa miaka miwili ijayo.
Benin inakuwa nchi ya pili mwaka huu baada ya Gambia, tkukutana zahama hiyo.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top