Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema nyota wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ ni mshambuliaji hatari na mwenye akili nyingi anapofika golini.
Phiri alimshuhudia Jaja akifunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kushinda 3-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Mzambia huyo, Phiri, alilimbia gazeti hili kuwa
licha ya watu wengi kumbeza Jaja, lakini ni mshambuliaji hatari
anapolikaribia lango na hapaswi kukabwa na mabeki legelege kwani wakati
wowote anaweza kufunga.
Phiri alisema Jaja ana nguvu licha ya kutokuwa na
kasi, lakini ana uamuzi mzuri anapokuwa karibu na lango, kitu ambacho
washambuliaji wengi hawana.
“Ni mchezaji mzuri, nimependa anavyofanya uamuzi
anapofika katika eneo la hatari, ana uamuzi wa haraka ambao wengi
hawategemei, licha ya kuwa ni mzito, lakini ni hatari na anapaswa
kuchungwa mno na mabeki.
Kikosi cha Phiri kitaivaa Yanga Oktoba 12, hivyo
amewataka mabeki wake kuwa makini watakapocheza na Yanga, ambao safu yao
ya ushambuliaji sasa itakuwa ikiongozwa na Jaja.
“Tunatakiwa kumuangalia sana siku tutakapokutana
na Yanga, inabidi tumfungie kazi, nimependa jinsi alivyofunga lile bao
la pili, washambuliaji wengi wasingeweza kufanya kile alichokifanya,
anaonyesha ana akili,” alisema Phiri.
Jaja alipata wakati mgumu katika mchezo huo
ulipoanza kiasi cha kufikia baadhi ya mashabiki wa Yanga kumpa presha
kocha Marcio Maximo amtoe, lakini kocha huyo Mbrazil ni kama aliweka
pamba masikioni huku akiamini mchezaji huyo atawanyamazisha.
Katika hatua nyingine, Maximo alisema alilazimika kutumia mifumo mitatu tofauti katika mchezo wao dhidi ya Azam.
“Nilianza na mfumo wa kukaba eneo la katikati
nikimtumia Said Juma aliyemudu vema nafasi hiyo na baadae kumtoa na
kumuingiza Hassan Dilunga naye alifanya kazi niliyomtuma ipasavyo,”
alisema Maximo.
Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya kuona wapinzani
wao wamepoteana katikati ya uwanja aliwataka wachezaji wake kupiga
mipira mirefu kwa kutumia kasi ya Mrisho Ngasa na Simon Msuva.
“Niliamua kumtoa Nizar (Khalfani) na kumuingiza
Msuva, ambaye ana kasi na aliimudu nafasi yake pia kama ilivyokuwa kwa
wengine walioingia,” alisema kocha huyo na kuongeza.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni