LOGO

Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mechi zake za kujipima ubavu katika kujiandaa na Ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuifunga KMKM mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa usiku huu kwenye wa Amaan visiwan Pemba.
 
Goli la wababe hao wa Tanzania bara lilifungwa na Mchezaji wao mpya Andrey Coutinho aliefunga kiufundi baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mrisho Ngasa katika dk ya 44 ya mchezo
Baada ya kupokea pasi hiyo umbali wa takribani mita 27, alizuga kama anatoa pasi, akiwa ameangalia upande mwingine aliusogeza mpira mbele na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.
Coutinho alishindwa kujizuia baada ya kufunga bao hilo na kuvua jezi yake kwa furaha huku wachezaji wenzake wakimshangilia kwa nguvu.
Hadi kipindi cha mapumziko Yanga ilikuwa mbele kwa bao dhidi ya KMKM
Kipindi cha pili KMKM walijitutumua na kupeleka mashambulizi mengi, lakini Yanga walikuwa imara zaidi.
Yanga walipoteza nafasi kadhaa lakini huku baadhi ya mashabiki wakiwa wameanza kutoka nje wakiamini Yanga imeshinda kwa bao hilo moja, Hussein Javu alifunga bao la pili kwa shuti kali pia, hiyo ikiwa ni dakika ya 90.
Jerry Tegete ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Javu alipoteza nafasi kadhaa za kufunga. Naye Hamisi Kiiza na Amos Abel, nafasi zao zilichukuliwa na Said Bahanuzi na Edward Charles.
Kikosi:
Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Yanga kukipiga Zanzibar na imeshinda yote.
Ilianza na Chipukizi na kushinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Jaja kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Ikapaa hadi Unguja na kuichapa Shangani kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Hivyo imeshinda mchezo mmoja kisiwani Pemba na miwili kisiwani Unguja.

Kikosi:
Deo Munishi ‘Dida’/Juma Kaseja (Dk46), Salum Telela/Said Juma (Dk46), Oscar Joshua/Amos Abel (Dk46)/Edward Charles (Dk70), Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Rajab Zahir (Dk46), Mbuyu Twite/Omega Seme (Dk46), Mrisho Ngassa/Simon Msuva (Dk46), Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (Dk46), Geilson Santana ‘Jaja’/Jerry Tegete (Dk46/Said Bahanuzi (Dk70), Haruna Niyonzima/Hamisi Thabiti (Dk46) na Andrey Coutinho/Hamisi Kiiza/Hussein Javu.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top