Klabu ya Arsenal ya England imefanikiwa kutinga rasmi kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi baada ya kuishinda Besiktas ya Uturuki kwa bao 1-0 kwenye Dimba la Emirates dakika ya 45.
Alikuwa ni mchezaji mpya aliejiunga na Arsenal akitokea Barcelona kwa ada ya paund milion 32 Alexis Sanchez , ndiye aliewapeleka Washika Bunduki hao hatua ya makundi kwa kufunga bao pekee katika mchezo huo akipokea pasi ya Jack Wilshere
Arsenal ililazimika
kufanya kazi ya ziada kuwafunga Waturuki hao ambao ilitoka nao sare kwao wiki iliyopita.
Licha ya kuwa pungufu baada ya beki wake Mathieu Debuchy kulambwa kadi
nyekundu, Arsenal ilipambana vilivyo.
Huu ni msimu wa saba mfululizo Arsenal inafanikiwa kucheza Ligi
ya Mabingwa Ulaya, michuano ambayo hugombewa na kila timu ya Ulaya.
VIKOSI
VIKOSI
Arsenal:
Szczesny 6.5, Debuchy 5.5, Mertesacker 6.5, Koscielny 7, Monreal 6,
Flamini 6, Oxlade-Chamberlain 6.5, Cazorla 6, Wilshere 7, Ozil 5.5
(Chambers, 76), Sanchez 7.5
Subs not used: Martinez, Coquelin, Rosicky, Podolski, Sanogo, Campbell
Goal Alexis Sanchez 45
Besiktas:
Zengin 6, Koybasi 6, Franco 6, Gulum 6.5, Motta 6, Hutchinson 6.5,
Ozyakup 5, Kavlak 7, (Uysal 76, 5); Pektemek 5.5 (Tosun 87), Ba 5.5,
Sahan 6 (Tore, 60, 5)
Subs not used: Gonen, Kurtulus, Sivok, Koyunlu
Bookings: Kavlak, Ozyakup, Franco, Hutchinson, Uysal, Tore.
Manager: Slaven Bilic, 6
Mwamuzi: Pedro Proenca 6.
Mahudhurio: 59,946
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni