Hatimaye Klabu ya Yanga imemfungulia
mashitaka mshambuliaji wake raia wa Uganda Emanuel Anold Okwi
Yanga imefikia uamuzi huo baada ya
kuonekana kutoridhishwa na mwenendo wa Okwi raia wa Uganda ambaye hata hivyo
ameishatua nchini akisubiri kujiunga na kikosi cha Yanga ambacho
kipo kambini
mjini Zanzibar.
Barua ya Yanga ya Agosti 25
iliyosainiwa na Katibu Mkuu, Beno Njovu, imetua kwenye Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) ikifafanua mambo mengi ikiwa ni pamoja na Okwi kukiuka mkataba
na Yanga kwa kufanya mazungumzo na klabu ya WadiGalde FC ya Misri.
Barua hiyo inaeleza Okwi amekiuka
vipengele vya Fifa, Caf na TFF kwa kufanya mazungumzo na timu hiyo ya Misri
ambayo tayari imeiandikia Yanga barua ikitaka kumnunua kwa dola 60,000 (zaidi
ya Sh milioni 95).
“Okwi aliwasiliana na mmoja wa viongozi
na kumuambia amefanya mazungumzo na timu ya Misri inamtaka, kiongozi akamuambia
aandike barua, kweli akafanya hivyo kupitia mwanasheria wake.
“Siku chache baada ya Yanga kupokea
barua, WadiGalde FC nayo ikaiandikia Yanga barua kuwa inamtaka kwa kitita cha
dola 60,000 ambazo zinalingana na zile zilizoandikwa kwenye barua ya
mwanasheria wake. Kulingana kwa kiwango cha fedha kunaonyesha walikuwa na
mawasiliano.
“Hili ni kosa kisheria kwa kuwa Okwi
bado ana mkataba na Yanga, angalau ingekuwa imebaki miezi sita angeweza kufanya
hivyo. Mwanasheria wake (Edgar Agaba) pia ameshiriki na tunaomba TFF kuwafungia
wote kujishughulisha na soka nchini,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
“Pamoja na kuwafungia, Okwi anatakiwa
kutulipa fidia ya dola 200,000 kwa kuchangia kutukosesha ubingwa pamoja na
kurudisha fedha zote alizolipwa za usajili ambazo ni dola 60,000 pia fedha zote
za mshahara,” ilifafanya zaidi sehemu ya barua hiyo.
Yanga imemtuhumu Okwi kwa kukosa mechi
saba kati ya 13 za mzunguko wa pili kitu kinachoonekana ni kama kuchukuliwa
fedha zake bure kwa kuwa Okwi hakuitumikia ipasavyo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni