LOGO



Hatimaye Klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam imemtema rasmi beki wake Hussein Butoyi raia Burundi baada ya kufanya majaribio ya wiki moja na kutomvutia kocha mkuu Patrick Phiri huku Beki wake Mkenya Benard Musoti akisalia klabuni hapo.
 
Mrundi huyo alimvutia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akiichezea Telecom ya Djibouti katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda mwezi huu.
Poppe akafanya mazungumzo na mchezaji huyo aje Dar es Salaam kufanya majaribio na kama angemvutia kocha Mzambia, angepewa mkataba.

Hata hivyo, baada ya wiki moja ya kufanya mazoezi na Simba SC visiwani Zanzibar pamoja na kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Kilimani City, kiwango chake hakijamvutia kocha Phiri.
Wakati dirisha la usajili la Simba SC linafungwa usiku wa leo, Kamati ya Usajili kwa pamoja na Kamati ya Ufundi zimeafikiana kuachana na Butoyi na kuendelea na Mosoti.
Maana yake wachezaji wa kigeni katika kikosi cha Simba SC watakuwa mabeki Mganda Joseph Owino, Mkenya Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera, mshambuliaji Amisi Tambwe na Mkenya Mkenya Paul Kiongera

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top