Wavuvi wawili wa china waliokuwa wamebakia rumande kwa miaka 5 baada ya wenzao kuachiwa mwaka 2011 nao wameachiwa huru katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Dar es salaam wavuvi hao walikuwa na kesi ya kuvua samaki bila kibali katika ukanda wa kiuchumi wa Tanzania.
Aidha mahakama imeamuru wavuvi hao warudishiwe mali zao ikiwemo meli yao samaki wao na pasi zao za kusafiria.
Hakimu mfawidhi Isaya Arufani aliwaachia watuhumiwa hao baada ya mkurugenzi wa Mashitaka DPP kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia kuendelea na mashitaka hayo na kuiomba Mahakama ya
kisutu kuwaachia huru wavuvi kutoka china maarufu kama wazee wa samaki
wa magufuli ,
Wahitakiwa hao ni Nahodha wa meli hiyo inayojulikana kama Tawaliq 1, Hsu chin Tai na wakala wa meli hiyo Zao Hanguing.
hivi haya si majanga kwa vyombo vyetu vya usalama Magufuli
samaki aliuza kwa mnada na meli ilianza kuzama sasa nani atabeba jukumu
la kwenda kuvua samaki za kuwarudishia? Na meli yao itanunuliwa na
nani?ama ndio kusema Waziri John Magufuli amelikoroga?
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni