LOGO

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Mexico Miguel Herrera amemwacha Straika wa Manchester United Javier Hernandez ‘Chicharito’ kwenye Kikosi cha Nchi hiyo kitakachocheza Mechi za Kirafiki Mwezi ujao.
Herrera amesema hakumchukua Chicharito kwa sababu anataka Mchezaji huyo apate muda wa kuangalia 
 hatima yake kwa kupata Klabu nyingine itakayompa Namba ya kudumu.
 
Huko nyuma, Kocha Miguel Herrera alishawahi kumtaka Chicharito ahame Man United ili apate Namba kwenye Timu ya Taifa.
Tangi ajiunge na Man United Chicharito aamekuwa hana Namba ya kudumu na mara nyingi ameingizwa kutoka Benchi ingawa kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England Wikiendi iliyopita Man United walipofungwa 2-1 na Swansea City Mchezaji huyo alianza Mechi hiyo.
Lakini kurejea tena kwa Robin van Persie, baada ya kuwa Likizo ndefu, kutamfanya Chicharito akose Namba Jumapili Man United watakapokuwa huko Stadium of Light kucheza Mechi ya Ligi na Sunderland.
Mexico inatarajiwa kucheza Mechi za Kirafiki na Bolivia na Chile huko Nchini USA Mwezi ujao na Kocha Herrera wa Mexico anatarajiwa kutaja Kikosi chake Wiki ijayo lakini ameanika Wachezaji 6 wanaocheza nje ya Nchi hiyo ili waombewe vibali toka Klabu zao.
Nae Wakala wa Chicharito, Eduardo Hernandez, amesema hadi sasa haijulikani kama Mchezaji huyo atabaki Man United au atahama.
Amesema: “Kwa sasa hatuna habari yeyote kutoka Manchester kama atabaki au kuhama.”

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top