LOGO


 How it's going to be: Balotelli mocked up in a Liverpool shirt in anticipation of his move to Anfield
NAHODHA wa zamani wa Liverpool Jamie Redknapp amedai kumsaini Fowadi wa Italy Mario Balotelli kunaweza kuiongezea Liverpool nguvu lakini pia ipo baala ya kuiletea majanga ya kuivuruga Timu hiyo.
Hivi sasa inasemekana Balotelli yupo Mjini Liverpool kupimwa afya yake ili kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan ya Italy.
Staa huyo wa Italy anasifika sana kwa umahiri wake wa kufunga Mabao safi lakini pia ana sifa mbaya ya ‘utovu wa nidhamu’ nje na ndani ya Uwanja.
Mastaa kadhaa wa zamani wa Liverpool, akiwemo Emile Heskey, wameonya kuwa Balotelli kutua Liverpool ni kukaribisha ‘majanga.’
Akiongea kuhusu Uhamisho wa Balotelli, Jamie Redknapp ameeleza: “Ni usajili mzuri lakini nimeshangazwa Liverpool kujiingiza kwenye njia hii. Hapa ni kucheza Bahati Nasibu kwa Meneja Brendan Rodgers kwani huyu Mchezaji anaweza kuivuruga Klabu!”
Akimfananisha Balotelli na Luis Suarez, Mchezaji wa Liverpool ambae amehamia Barcelona Mwezi uliopita, Redknapp alisema: “Ingawa Suarez alikuwa na kasoro nyingi lakini alijituma Uwanjani. Lakini Balotelli wakati mwingine anaonyesha kutojali na kutojituma Uwanjani na hili kwa Klabu kama Liverpool ambayo Washabiki wake wanataka kila Mtu ajitume Asilimia 100 kila Siku ni ngumu! Lazima afanye bidii!”
Redknapp pia aliwakumbusha maneno aliyosema Mchezaji mwingine ambae nae husemwa ni mkorofi, Adel Taraabt, ambe Msimu uliopita alikuwa kwa Mkopo AC Milan wakicheza pamoja na Balotelli, alipoonya: ‘Kama unadhani mimi mbaya, lazima umuone Balotelli!’

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top