LOGO




(Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho )

Ukizungumzia walinda mlango mahiri waliowahi kutokea duniani basi si rahisi kutomtaja Petr Cech(miaka 32) wa Chelsea na timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech. Cech amewahi kutwaa tuzo ya mlinda mlango bora wa dunia mwaka 2005 ikiwa ni mwaka mmoja mbele tokea ajiunge na klabu ya Chelsea akitokea Rennes ya Ufaransa. Mbali na tuzo hiyo bado aliendelea kutwa tuzo mbalimbali kuthibitisha ubora wake Mlinda mlangoo bora wa ligi kuu Uingereza, Mchezaji bora wa Czech, Mlinda mlango bora klabu bingwa ulaya na mchezaji bora wa Chelsea wa mwaka. (Baadhi tu ya zile tuzo alizowahi kuzitwaa)

Petr Cech amecheza zaidi ya michezo 450 akiwa chaguo la kwanza kwenye klabu ya Chelsea tokea 2004. Mwaka 2011 Chelsea ilimsajili mlinda mlango chipukizi na kumsainisha mkataba wa miaka 5. Kinda huyo si mwingine ni Thibaut Courtis raia wa Ubelgiji. 2011 alicheza mchezo mmoja tu akiwa na klabu yake mpya ya Chelsea, na baadae ndani ya mwaka huo huo alitolewa kwa mkopo kuichezea klabu ya ATletico Madrid ya Uhispania. Kutokana na umahiri wa mlinda mlango Petr Cech , Courtis aliendelea kutumika kwa mkopo Atletico Madrid kwa miaka mitatu na kucheza michezo 111 mingi akiwa kama chaguo la kwanza chini ya kocha Diego Semion.

Courtis alifanikiwa kucheza kwa mkopo Atletico kwa misimu mitatu ya mafanikio ni kuonesha uwezo wa hali ya juu sana licha ya kuwa na umri mdogo (miaka 22 kwa sasa). Kiwango cha Courtis kilichangia Atletico Madrid kutwa taji la ligi kuu Uhispania 2014, kufika fainali ya klabu bingwa ulaya 2014, kutwa taji la EUROPA LEAGUE na Copa De rey. Courtis tayari ameshaonja uzoefu wa ligi mbili kubwa za ulaya. Leo hii mkataba wake wa mkopo na Atletico umekwisha malizika na amerudi kwenye klabu yake ya Chelsea 2014.

Ujio wa Courtis Chelsea, umeweka kibarua cha mlinda mlango mkongwe Cech matatani. Kocha wa Chelsea Jose Mourihno ameonesha nia ya kumfanya Courtis kuwa chaguo lake la kwanza jambo ambalo litampa nafasi finyu Petr Cech na huenda asiridhike nalo. Courtis alikuwa chaguo la kwanza kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza wa Chelsea dhidi ya Burnley huku Cech akisugua bechi.Klabu ya PSG ndiyo inayoongoza kwa nia ya kutaka kunasa saini ya mkongwe huyo mwenye miaka 32 kwa sasa. 

HILI NDILO TAMKO RASMI LA KOCHA JOSE MOURIHNO KWA MLINDA MLANGO PETR CECH.

"Cech kama atataka kuihama klabu milango iko wazi. Japo kuwa mpaka sasa hajaonesha nia ya kuihama klabu hiyo" Alisema Mourihno. Mourihno hakusita kuonesha heshima yake na kumthamini mlinfa mlango huyo kwa kusema bado ni mchezaji wetu na tunamheshimu ya yote aliyoifanyia klabu. Mourihno alisisitiza kuwa yeye huwa hazungumzii wachezaji kubaki au laa, ila klabu huwa inatoa maamuzi na yeye analiheshimu hilo. 
Kauli ya kuweka mlango wazi kwa mlinda mlango huyo itazidi kuwafanya PSG waongeze kasi ya kutaka kumwania mchezaji huyo.

Mourinho "Tuna walinda mlango wawili mahiri duniani" Aliongeza. Mourihno alipoulizwa juu ya suala la kumpa nafasi mchezaji huyo kama atabakia klabuni hapo alijibu kwa urahisi tu kuwa, haoni tabu kumchezeasha mchezaji huyo kama mzunguko wa wachezaji ulivyo klabuni, pia hatojali ni mashindano gani atampanga.



(Walinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtis (kushoto) na Petr Cech (kulia))

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top