LOGO


 CAF-LOGI14A



















SHIRIKISHO LA SOKA AFRICA limewanyang’anya Libya Uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za Mwaka 2017, AFCON 2017.
CAF imeondoa Uenyaji huo kutokana na Vita inayoendelea Nchini humo ambayo imesababisha kutojengwa kwa Viwanja vilivyoahidiwa kwa ajili ya Fainali hizo zinazoshirikisha Nchi 16.
Sasa CAF imetoa nafasi kwa Nchi nyingine za Afrika kuwasilisha maombi yao ya kuwa Wenyeji na Maombi hayo yanatakiwa yawafikie CAF kabla ya Septemba 30.
Awali Libya walitakiwa wawe Wenyeji wa Fainali hizo Mwaka 2013 lakini kutokana na Vita hiyo wakabadilishana na South Afrika waliokuwa Wenyeji wa AFCON 2013 na wao Libya kuchukua AFCON 2017.
Mashindano yajayo ya AFCON 2015 yatafanyika huko Nchini Morocco Januari 2015 na sasa Nchi zipo hatua ya Makundi kusaka Nchi 15 zitakazojumuika kwenye Fainali na Wenyeji Morocco.
AFCON 2015
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Congo
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Lesotho
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Sierra Leone
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Botswana

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top