KHEDIRA ATOA KAULI TATA KUHUSU HATIMA YAKE MADRID
(Kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira )
Baada ya kuhusishwa na uvumi wa kuhamia Manchester United ya Uingereza siku hizi za karibuni, Kiungo huyo wa Ujerumani ametoa kauli iliyozua maswali mengi kuhusu hatma yake na klabu yake ya sasa ya Real Madrid.
Khedira alinukuliwa akisema kuwa "Right now I'm a little out of Real Madrid,". Maneno haya ya lugha ya kiingereza yanamaana ya kuwa "kwasasa yupo nje kidogo na Real Madrid" Sio nje kwa maana ya kuwa nje ya jengo la klabu ya Real Madrid, La hasha bali yupo nje kidogo na Real Madrid akimaanisha kuhusu hatma yake kiujumla. Khedira bado anao mkataba na Madrid utakao kwisha 2015.
Ujio wa nyota mjerumani mwenzake, Toni Kroos umeongeza hofu ya kumfanya khedira apate nafasi finyu kwenye safu ya kiungo. Klabu inayomwania Sami Khedira kwa ukaribu ni klabu ya Manchester United ya Uingereza pekee. Ila zilizowahi kuhusishwa na sakata la kutaka saini ya kiungo huyo ni pamoja na Arsenal na Chelsea zote za Uingereza.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni