LOGO

Mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kagame cup leo yanafikia tamati kwa mchezo wa final na wa kutafuta mshindi wa tatu mechi ya finali itawakutanisha APR ya Rwanda na El Merreikh ya Sudan itakayochezwa Uwanja wa Nyamirambo huko Kigali, Rwanda majira ya saa 10:00 kwa saa za kibongo. kabla ya mechi ya finali kutakuwa na mechi ya kumtafuta mshinda wa tatu kati ya Police ya Rwanda na KCC ya Uganda kwenye mchezo utakaochezwa  kwenye Uwanja wa Nyamirambo majira ya saa 7:30 kwa saa za kitanzania
 
CECAFA tayari imethibitisha kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ndie atakuwa Mgeni rasmi hii Leo kwenye Fainali ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na ya Kati, Kagame Cup, kati ya
Habari za Rais Kagame, ambae ndie Mlezi wa Kombe hili, kuhudhuria Fainali ya Leo zilithibitishwa na Rais wa CECAFA, Leodgar Tenga, ambae alikuwa pamoja na Makamu wake Lawrence Mulindwa na Katibu Mkuu wao , Nicholas Musonye, walipoongea na Wanahabari Jana Usiku kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Soka la Rwanda, FERWAFA.
Vile vile CECAFA imethibitisha kuwa Rais Kagame ameshawakabidhi zawadi kwa Washindi ambazo ni Dola 60,000 kwa Bingwa, Dola 30,000 kwa Mshindi wa Pili na Dola 20,000 kwa Mshindi wa 3.
Pia, Bingwa wa Kagame Cup atapewa Kombe jipya kabisa ambalo ni mchango wake binafsi Makamu wa Rais wa CECAFA, Lawrence Mulindwa.
Mechi hii itachezwa kwa Dakika 90 na ikiwa ni Sare Mikwaju ya Penati 5 itapigwa kusaka Mshindi.
Kwenye Fainali, Timu zikiwa Sare baada ya Dakika 90, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa na ikiwa bado Sare Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati tano tano.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top