MSHAMBULIAJI
wa Cameroon, Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu
kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu
yake JS Kabylie imesema.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na kitu hicho kigumu mwishoni mwa
mchezo kati ya JS Kabylie na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Taarifa
katika tovuti ya Kabylie jana imesema: "Wizara ya Mambo ya Ndani na
Serikali ya Nyumbani, kupitia Waziri Tayeb Belaiz, imeagiza uchunguzi wa
wazi uanze mara moja juu ya tukio hilo lililosababisha kifo cha Albert
Ebosse.
Ebosse aliifungia bao Kabylie katika mechi hiyo iliyoisha kwa kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa USM Alger.
WASIFU MFUPI WA EBOSSE |
---|
JINA KAMILI | Albert Dominique Ebossé Bodjongo Dika | ||
---|---|---|---|
TAREHE YA KUZALIWA | October 6, 1989 | ||
MAHALI ALIPOZALIWA | Douala, Cameroon | ||
TAREHE ALIYOFARIKI | August 23, 2014 (aged 24) | ||
MAHALI ALIPOFARIKI | Tizi Ouzou, Algeria | ||
UZITO | 1.85 m (6 ft 1 in) | ||
NAFASI ANAYOCHEZA | Forward | ||
Senior career* | |||
MIAKA | TIMU ALIZOCHEZA | MECHI | MAGOLI |
2008-2010 | Coton Sport FC | ||
2010-2011 | Unisport Bafang | ||
2011-2012 | Douala AC | 10 | (9) |
2012-2013 | Perak FA | 16 | (11) |
2013–2014 | JS Kabylie | 31 | (17) |
TIMU YA TAIFA | |||
2009 | Cameroon U20 | ||
2009–2014 | Cameroon | 6 | (0) |
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni