(Mchezaji mpya wa Napoli, Jonathan De Guzman.)
Baada ya kuitumikia klabu ya Swansea city ya Uingereza kwa mkopo wa miaka miwili kutoka Villareal ya Uhispania, Kiungo huyo sasa amwaga wino klabu ya SC Napoli ya Italia.(kiasi hakikutajwa) De Guzman ambae alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 kuiwakilisha taifa la Uholanzi kwenye michuano ya kombe la Dunia huko Brazil na kucheza mara kwa mara, amesaini mkataba wa miaka minne utakao mfanya awe mchezaji halali wa Napoli mpaka 2018.
Akiwa Swansea amecheza michezo 59 ligi kuu Uingereza na kufunga mabao 9.
(De Guzman akikaribishwa na kocha wa Napoli, Rafael Benitez)
(De Guzman akiwa na jezi ya klabu yake ya zaman,Swansea aliyeitumikia kwa miaka miwili kwa mkopo akitokea Villareal ya Uhispania)
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni