LOGO


Timu ya soka ya Dar Young African imeanza vizuri kwenye mechi yake ya kirafiki kwa kuifunga Chipukizi FC ya Zanzibar kwa goli 1 kwa nunge .
 
 JAJA
Mechi hiyo inakuwa ya kwanza kocha Marcio Maximo tangia ajiunge na Yanga SC mwez uliopita.
Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba uliochezwa kwenye Uwanja wa Gombani mjini hapa.

Bao la pekee Yanga katika mechi hiyo lilifungwa katika dakika ya 6 na mshambuliaji wake Mbrazil, Jaja.
Jaja alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kuruka juu na kuuwahi mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Maximo alikuwa akibadili wachezaji mfululizo akionyesha alikuwa amepania kuona jambo fulani.
Hiyo ndiyo mechi ya kwanza kwa Yanga kucheza ikiwa chini ya Maximo ambaye awali alikataa mechi za kirafiki akitaka kwanza kujenga kikosi.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top