UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya
Tanga umemfungia aliyekuwa beki wa kushoto Abdi Banda kucheza mpira
wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukosa
nidhamu na kusaini mikataba katika vilabu viwili tofauti.
Adhabu hiyo itahusisha
kutokucheza mechi zozote ikiwemo zile za kirafiki kutokana na kukiuka
makubaliano aliyoingia na klabu hiyo ya Coastal Union wakati aliposajiliwa.
Akitoa taarifa hiyo kwa
waandishi wa habari leo,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa
uongozi umeamua kumpa adhabu hiyo kwa kukosa nidhamu pale aliposaini
mkataba mwingine na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam wakati akijua tayari ana
mkataba wa miaka mitatu na timu ya Coastal Union.
El Siagi alisema kuwa mchezaji
huyo alikuwa amebakiza miaka miwili kucheza timu ya Coastal Union na hivi sasa
yupo katika mikataba miwili kwa timu mbili tofauti ambazo zinashiriki ligi moja.
“Ki ukweli
hali hii hatuweza kuivumilia ndio maana tumeamua kuchukua hatua hiyo kali ili
iweze kuwa fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama hii “Alisema Katibu
El Siagi.
Alisema kuwa kutokana na hali
hiyo mchezaji huyo atakuwa amevunja sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa
miguu hapa nchini na kulitaka shirikisho la soka kutoa ushirikiano katika
maamuzi hayo.
shaffihdauda
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni