Alikuwa ni kiungo wake mpya alietokea Mtibwa Shaaban Kisiga Malone alieifungia Simba goli la kuongoza dakika ya 14 ya mchezo kwa mkwaju wa penaltybaada ya kiungo Uhuru Suleiman kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Kilimani City Rashidi Ally.
Kipindi cha pili ilifanya mabadiliko kwa kutoa kikosi kizima nje isipokuwa Shabani Kisiga na mnamo dakika ya 76 Kilimani City ilisawazisha kuputia kwa
Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao moja, lililofungwa kwa penalti na kiungo wake aliyerejea kikosini, Shaaban Kisiga ‘Malone’ dakika ya 14. Penalti hiyo ilifuatia kiungo Uhuru Suleiman kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Kilimani City, inayocheza Ligi Daraja la Pili wilaya Mjini, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Rashid Ally. Kipindi cha pili, kocha Phiri alibadilisha karibu kikosi kizima kilichoanza, kasoro Kisiga pekee. Kilimani ilisawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Hassan Ameir aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Adam Abdallah baada ya kuwahadaa mabeki wa Simba SC.
Zikiwa zimebaki dakika 7 mpira uishe Haruna Chanongo alieingia akitokea Benchi aliifungia Simba SC bao la ushindi na kuwa hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Simba SC 2-1 Kilimani City.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Nassor Masoud ‘Chollo’/Miraj Adam, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/Said Ndemla, Hussein Butoyi/Joram Mgeveke, Uhuru Suleiman/Abdallah Seseme, Amri Kiemba/Haroun Chanongo, Amisi Tambwe/Elias Maguri, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Abdi Banda.
Kilimani City; Hafidh Ally, Mzee Abdallah, Mzee Kheri, Kassim Omar, Mohammed Hajji, Lukman Ayoub, Abdulwahid Muhsin, Adam Abdallah/Hassan Shaame, Bakari Bakari, Rashid Ally na Matar Mohammed/Mashi Shehe.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni