LOGO

Ligi kuu soka nchini England inaendelea tena leo kwa kushuhudia mchezo mmoja katiya mabingwa wa England, Manchester City, chini ya Meneja wao Manuel Pellegrini, watacheza na Liverpool iliyochini ya Brendan Roggers kwenye dimba la Etihadi Jumatatu Usiku majira ya saa 4:00 kwa saa za kitanzania.
Timu zote ziliweza kushinda mechi zao za ufunguzi wa ligi ambapo leo ni mechi ya pili ya kila timu kwa ajili ya kusaka point 6 
 
Man City walianza Ugenini huko St James Park na kuifunga Newcastle Bao 2-0 na Liverpool kuanza kwao Anfield na kushinda kwa mbinde Bao 2-1 walipoifunga Southampton huku Bao la ushindi likifungwa mwishoni na Daniel Sturridge.
Wakati Liverpool wametumia zaidi ya Pauni Milioni 100 kuimarisha Kikosi chao kwa Wachezaji wengi 
wapya, Man City wao Kikosi chao kwa ujumla ni kile kile cha Msimu uliopita.
 
Hali za Timu
Mastraika wa Manchester City Edin Dzeko na Stevan Jovetic wanaelekea wataanza Mechi hii kwani Sergio Aguero bado hajawa fiti kucheza Mechi kwa Dakika 90 kufuatia kuwa Majeruhi.
Pia City wanaweza wasimchezeshe Mchezaji wao mpya kutoka FC Porto ambae ni Beki wa Kimataifa wa France, Eliaquim Mangala, kutokana na kutozea mikikimikiki ya England.
Liverpool huenda wakawatumia wapya wao, Kiungo wa Serbia Lazar Markovic na Beki Alberto Moreno, kwenye Mechi hii muhimu.
Lakini Uwanjani Etihad, Man City ni kiboko na Msimu uliopita waliichapa Liverpool Bao 2-1 na Timu pekee zilizoambua ushindi hapo ni Bayern Munich, Barcelona, Chelsea na Wigan.
mara walivyo kutana hivi karibuni
-Manchester City hawajafungwa Nyumbani kwao na Liverpool katika Mechi 5 zilizopita kwa Kushinda 3 na Sare 2.
-Msimu uliopita, City walishinda Etihad 2-1 na Liverpool kushinda kwao Anfield 3-2.
-Mara ya mwisho kwa Liverpool kupata ushindi Nyumbani kwa City ni Oktoba 2008 waliposhinda 3-2.
VIKOSI VINATARAJIWA:
MAN CITY: Joe Hart, Clichy, Kolarov, Kompany, Demichelis, Fernando, Yaya Toure, Nasri, Aguero, Silva, Dzeko
LIVERPOOL: Mignolet, Manquillo, Skrtel, Lovren, Johnson, Gerrard, Lucas, Sterling, Henderson, Coutinho, Sturridge
REFA: Michael Oliver

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top