LOGO


Mashindano ya klabu bingwa Afrika Masharikim na kati Kagame CUP imefikia tamati leo jijini Kigali nchini Rwanda kwa klabu ya EL Merreikh ya Sudan imetwaa ubingwa  jioni ya leo baada ya kuwafunga wenyeji, APR bao 1-0 Uwanja wa Amahoro,

El Merreikh ilipata bao lake lililoipa ushindi kwa kupitia mshambuliaji wake kimataifa wa Kenya, Alan Wanga aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 24 akimalizia krosi ya Ragi Abdallah.
Hilo linakuwa taji la michuano hiyo kwa Merreikh iliyoitoa Azam FC katika Robo Fainali kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0, awali ikibeba taji mwaka 1986 na 1994.
Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliotangulia leo, Polisi ya hapa iliifunga KCC ya Uganda kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya 0-0.
Kwa ushindi huo, El Merreikh wamezawadiwa dola za Kimarekani 30,000 wakati APR, imepata dola  20,000 kwa kushika nafasi ya pili wakayi Polisi iliyomaliza nafasi ya tatu imepata dola  10,000.
Kagame cup lilianza agost 8 mwaka huu likishirikisha timu 14 kutoka ukanda huu wa  Afrika Mashariki na Kati na bingwa kuwa El Merreikh.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top