Kocha wa Simba, Patrick Phiri amemteua beki Joseph Owino kuwa nahodha mpya wa timu hiyo na atasaidiwa na kiungo mkongwe, Shaaban Kisiga.
Kabla ya kutwaa uongozi huo, Owino ambaye ni raia
wa Uganda alikuwa nahodha wa muda wa timu hiyo, cheo alichokitwaa baada
mtangulizi wake, Said Nassor ‘Cholo’ kuumia na kukaa nje ya dimba kwa
muda mrefu.
Akizungumza kutoka Zanzibar iliko
kambi ya Simba, Phiri alisema amewapa Owino na Kisiga majukumu hayo
baada ya kuridhishwa na mwenendo wao ndani na nje ya uwanja.
“Uteuzi huu nimeufanya kwa kuzingatia mwenendo
mzuri wa wachezaji hawa kuanzia ndani ya uwanja hadi nje, lakini pia
uzoefu wao,” alisema kocha huyo Mzambia ambaye alipewa jukumu la kuinoa
tena timu hiyo mapema mwezi huu.
“Hakuna shaka hata wachezaji wengine wamekubaliana na uteuzi huu na nina imani watakuwa viongozi wazuri mbele ya wenzao.”
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni