Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji amesema Simba wamekurupuka katika suala la Emmanuel Okwi.
Manji
amesema Simba wamefanya haraka kumsajili mchezaji ambaye
ana mkataba na Yanga.
“Okwi
bado ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na Yanga lakini ana kesi na Yanga.
“Simba
wamekiuka sheria za Fifa kwa kumsajili mchezaji ambaye ana mkataba. Sisi tumemfungulia
Okwi mashitaka akiwa bado mchezaji wetu na mkataba wetu naye haujaisha.
“Sasa
walishindwa hata kutuuliza kuliko kukurupuka hivi,” alihoji Manji.
“Leo
nitazungumza na waandishi, unaweza ukanisikiliza na kupata ninachosema lakini
nakuhakikishia Simba wamekurupuka na wamevunja sheria na kanuni za Fifa
kumsajili mchezaji mwenye mkataba na mtu mwingine.
“Sikuona
sababu ya wao kujiingiza matatizoni,” alisema Manji ambaye anazungumza na
waandishi leo saa tano asubuhi kuhusiana na suala hilo la Okwi.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni