LOGO

TANZANIA inajiandaa kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017, muda mchache baada ya libya kutolewa kutokana na machafuko.
rais
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba wana uwezo na wako tayari kuwa wenyeji wa fainali hizo- hivyo wataomba.
“Tutaomba kuwa wenyeji wa AFCON ya 2017 kuziba pengo la Libya, tuko tayari na tuna uwezo, tunatarajia sapoti kubwa ya Serikali na wadau wengine wa Tanzania katika hili,”amesema Malinzi.
Libya imeamua kujitoa kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo- hivyo kuhofia mazingira ya kiusalama.
Awali, Libya ilipewa uenyeji wa fainali za mwaka 2013, lakini ikajitoa kwa sababu kama hizo na Afrika Kusini ikapewa nafasi hiyo- huku makubaliano yakifikiwa wao wataandaa AFCON ya mwaka 2017.
Jumamosi ikatangazwa tena, Libya imejitoa baada ya viongozi wa nchi hiyo kukutana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou.
CAF ikasema jitihada za kumsaka mbadala wa Libya zinaanza mara moja- maana yake kujitokeza kwa Tanzania ni ahueni kwao.
Kwa sasa, Tanzania inaweza kabisa kuwa mwenyeji wa fainali hizo kwa kuwa ina viwanja visivyopugua vitatu vyenye sifa, ingawa vingine vitahitaji marekebisho madogo.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hakuna shaka una sifa zote, wakati CCM Kirumba mjini Mwanza na Sheikh Amri Abeid Arusha vitahitaji marakebisho kidogo.   
Iwapo Tanzania itafanikiwa kupata uenyeji wa fainali za mwaka 2017, itakuwa imefuzu moja kwa moja kucheza michuano hiyo bila kupitia kwenye hatua ya mchujo.
Na hiyo itakuwa mara ya pili kihistoria kushiriki AFCON baada ya 1980 mjini Lagos, Nigeria wakati huo bado michuano hiyo ikiitwa Kombe la Mataifa ya huru ya Afrika.
Tanzania ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji Nigeria, Ivory Coast na Misri na ikashika mkia. Ilifungwa 3-0 na Ngeria, 2-1 na Misri na kutoka sare ya 1-1 na Ivory Coast.  
Yapo matumaini makubwa Tanzania ikafanikiwa kupewa yenyeji wa michuano hiyo mwaka 2017, kutokana na uhusiano mzuri baina ya Hayatou na rais wa sasa wa TFF, Malinzi. Kwa ujumla, FIFA na CAF zina imani kubwa na utawala wa Malinzi.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top