STRAIKA wa Italy Mario Balotelli Leo hii amekamilisha Uhamisho wake wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan na kutua Liverpool.
Balotelli, mwenye Umri wa Miaka 24 na ambae alicheza Ligi Kuu England akiwa na Manchester City, amesaini Mkataba wa muda mrefu na Liverpool lakini Usiku huu hatacheza Mechi ya Ligi huko Etihad kati ya Man City na Liverpool.
Balotelli aliihama Man City Miezi 17 iliyopita baada ya kuwa nao kwa Misimu Mitatu na kufunga Bao 30 na kurudi kwao Italy kuichezea AC Milan.
Licha ya Wachambuzi wengi huko England kuhoji na kuhofia Uhamisho wa Balotelli kutua Anfield, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, amesema Uhamisho huu ni manufaa makubwa kwa Liverpool na kusisitiza Dili hii ni biashara safi sana kwao.
Akiwa na Liverpool, Balotelli atavaa Jezi Namba 45.
Akiongelea ujio wake Liverpool, Mchezaji huyo mwenye vituko nje na ndani ya Uwanja alikiri kuwa kuondoka kwake England ilikuwa ni makosa.
Amesema: “Nina furaha kuwa hapa kwa sababu niliondoka England kwa makosa. Liverpool ni moja ya Timu bora hapa England na Soka hapa ni zuri sana!”
LIVERPOOL - WACHEZAJI WAPYA MSIMU HUU:
-Rickie Lambert (Southampton)
-Adam Lallana (Southampton)
-Emre Can (Bayer Leverkusen)
-Lazar Markovic (Benfica)
-Dejan Lovren (Southampton)
-Divock Origi (Lille)
-Javier Manquillo (Atletico Madrid)
-Alberto Moreno (Sevilla)
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni