LOGO

Mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, mwaka huu yamepangwa kufanyika Novemba mwishoni nchini Ethiopia, imeelezwa jana jijini hapa.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Leodegar Tenga, alisema jana kuwa Ethiopia imeshathibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yanayoshirikisha timu za taifa za nchi wanachama.

Tenga alisema baada ya kumalizika kwa mashindano ya ngazi ya klabu (Kombe la Kagame) hapo jana Jumapili, sasa ni wakati wa nchi kuandaa timu zao za taifa ili kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Aliongeza kuwa, anatarajia pia kuona ushindani ulioonyeshwa katika ngazi ya klabu unahamia kwenye timu za taifa.

"Baada ya mashindano ya klabu kumalizika, sasa macho yetu ni kuelekea Ethiopia, tunahitaji kuona ushindani na changamoto kwa ajili ya kukuza kiwango cha soka letu," alisema kwa kifupi mwenyekiti huyo.

Tenga aliongeza kuwa, mbali na mashindano hayo, pia Cecafa mwaka huu imeandaa michuano ya vijana ya umri chini ya miaka 23 na maandalizi yake yanakwenda vizuri.

Alisema michuano hiyo itafanyika nchini Sudan na wachezaji watakaoruhusiwa ni wenye umri husika kwa kuzingatia vipimo.

Mwaka jana Kenya ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Chalenji na timu yao ya Harambee Stars ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo.

Bingwa wa michuano hiyo hupata Dola za Marekani 30,000, wa pili Dola za Marekani 20,000 na wa tatu Dola za Marekani 10,000 sawa za zawadi zinazotolewa katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top