Klabu ya Everton hatimaye imemsaini Straika wa Cameroon Samuel Eto'o kwa Mkataba wa Miaka Miwili.
Eto’o, mwenye Miaka 33, amejiunga kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Chelsea wa Mwaka mmoja kumalizika.
Liverpool walikuwa wakimwania lakini baadae wakaamua kumchukua Matrio Balotelli na hivyo njia ikawa wazi kwake kujiunga na Everton.
Eto’o, ambae amewahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika mara 4, alijiunga na Chelsea kutokea Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala Msimu uliopita na kuifungia Bao 12 katika Mechi 34 alizocheza.
Eto’o alianzia Soka lake huko Real Madrid lakini alijenga jina lake akiwa na Mahasimu wao FC Barcelona.
Akiwa na Barcelona, Eto’o alitwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI mara mbili, Miaka ya 2006 na 2009 huku akipiga Bao katika Fainali hizo zote, na La Liga mara 3 na kisha kuhamia Inter Milan Mwaka 2009 na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Msimu wake wa kwanza tu.
Jana Nchi yake Cameroon ilimtema toka Timu yao ya Taifa baada ya kuichezea kwa Miaka 17.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni