KLABU
ya Barcelona imekamilisha usajili wa beki wa kulia wa kibrazil Douglas Pereira kutoka
Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, Barcelona wametoa taarifa hiyo jana
Uhamisho
unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo
mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika
klabu yake mpya.
Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.
Beki la kushambulia: Beki huyo amefunga mabao sita katika mechi 124
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni