UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUENDELEA ARSENAL DIMBANI KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA MAKUNDI UEFA DHIDI YA BESKTAS YA DEMBA BA
Hatua ya mchujo kwa ajili ya kupata timu zitakazo cheza makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu huu yanaendelea leo usiku majira ya 3:45 kwa kushuhudia timu mbalimbali zikijitupa uwanjani kusaka tiketi hiyo.
Klabu ya Arsenal wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya Uturuki Besiktas baada ya sare ya kutofungana kwa mechi ya awali iliyochezwa huko Istambul nchini Ugiriki.
Besktas wakitoa droo yoyote ya magoli watakuwa wametinga hatua hiyo ya makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo Droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi.
Arsenal wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae alipewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul.
Pia Arsenal itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na vile vile kumkosa Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.
Kukosekana kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo au Lukas Podolski au hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama Sentafowadi au ikibidi, Arsene Wenger kumtumia Joel Campbell.
Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.
VIKOSI VINATARAJIWA:
ARSENAL: Szczesny; Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal; Flamini, Wilshere; Oxlade-Chamberlain, Ozil, Cazorla; Sanchez
BESIKTAS: Zengin; Koybasi, Franco, Gulum, Motta; Ozyakup, Uysal, Kavlak, Sahan, Pektemek; Ba
Mechi za leo Jumatano August 27
Arsenal v Besiktas [0-0]
Athletic Bilbao v Napoli [1-1]
Bayer 04 Leverkusen v FC Copenhagen [3-2]
Ludogorets Razgrad v Steaua Bucharest [0-1]
Malmö FF v FC Red Bull Salzburg [1-2]
Mechi z
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni