
Yanga imejiona imelamba dume kwa
kumsajili Deus Kaseke aliyemaliza mkataba wake Mbeya City, sasa timu
hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Mbeya, inamsajili Hamis
Kiiza.
Kiiza alitamba akiwa na Yanga kabla ya kuachwa mwanzoni mwa msimu uliopita na kisha kutimkia Oman kabla ya kurejea kwao Uganda.
Mmoja wa maofisa wa Mbeya City
amelithibitishia Championi Jumamosi kuwa, wapo katika hatua nzuri za
kumsajili Kiiza, tayari kwa msimu ujao.
“Kila kitu kinakwenda vizuri na
Kiiza anaelekea kusaini mkataba wa kuichezea Mbeya City msimu ujao,
tunataka kuimarisha timu baada ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji,”
alisema bosi huyo mwenye sauti Mbeya City.
Baadhi ya wachezaji walioondoka
Mbeya City ni Kaseke aliyejiunga Yanga, Peter Mwalyanzi (Simba), Themi
Felix (Kagera Sugar) na Paul Nonga na Anthony Matogolo waliojiunga na
Mwadui FC ya Shinyanga.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni