
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans
van der Pluijm tayari ameshawasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini
Ghana alikokuwa kwa mapumziko mara baada ya kumalizika kwa msimu wa
ligi kuu Tanzania bara 2014-2015 ambapo alikiongoza kikosi cha
wanajangwani kutwaa ubingwa wa ligi.
Pluijm amerejea kuanza majukumu
ya kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya michuano mbalimbali
inayoikabili timu hiyo ikiwa ni pamoja na mashindano ya Kagane Cup, ligi
kuu Tanzania bara na ile ya vilabu bingwa barani Afrika
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni