Shirikisho
la soka nchini Uingereza FA limesema kuwa halina haja ya kuandaa kombe
la dunia la mwaka 2018 ama lile la mwaka 2022 nchini Qatar iwapo mataifa
yanayoandaa yatapokonywa fursa hiyo.
Maafisa wa mashtaka wa
Uswizi wanachunguza zabuni za michuano hiyo ,ijapokuwa FIFA inasema kuwa
hakutakuwa na ushindani mwengine wa kutolewa kwa zabuni hizo.Katibu wa utamaduni nchini Uingereza John Whittingdale anasema kuwa Uingereza huenda ikachukua maandalizi ya kombe hilo iwapo itaombwa kufanya hivyo.
Lakini afisa mkuu wa shirikisho la FA Martin Glenn amesema kuwa Uingereza haina haja.
Akizungumza na SkyNews,Glenn ameongezea kwamba michuano hiyo ya mwaka 2018 itaandaliwa na Urusi kwa njia nzuri.
bbc swahili
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni