Azam
FC inatarajia kuanza mazoezi jumanne ijayo tarehe 16 kujiandaa ligi kuu
msimu wa 2015/16 na mashindano ya kombe la Kagame litakalotimua vumbi
jijini Dar es Salaam kuanzia July 11 mwaka huu. Kikosi cha Azam FC chini
ya Kocha mwenye uzoefu na ligi ya Tanzania na klabu ya Azam FC Stewart
Hall aliyerejeshwa kukinoa kikosi hicho kimedhamiria kufanya makubwa
msimu huu. Azam FC ambayo imewaruhusu wachezaji wake watatu kuondoka
ambao ni Amri Kiemba, Gaudence Mwaikimba na Wandwi Jackson ipo katika
mawindo ya wachezaji kadhaa wa ndani na nje ya nchi ili kuimarisha
kikosi chake na kukiongezea nguvu. Kinachosubiriwa ni taarifa rasmi toka
TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni, hilo likishajulikana, uongozi
utakaa na Benchi la ufundi kisha kuamua ni wachezaji gani toka nchi gani
wanaohitajika kuongeza nguvu alisema Mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad
kawemba katika mahojiano yake na tovuti ya klabu
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni