
Bayern Munich itapigana hadi mwisho ili kupindua kipigo cha 3-0 walichopewa na Barcelona katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, huko Nou Camp, Spain Wiki iliyopita.
Timu hizi zinarudiana Mjini Munich ndani ya Allianz Arena Jumanne Mei 12 na Bayernn wamepiga mbiu kuitisha vita waliyoshinda Raundi iliyopita ya UCL baada kuchapwa 3-1 na FC Porto huko Ureno katika Mechi ya Kwanza na kuinyuka Timu hiyo 6-1 ndani ya Allianz Arena.
Kocha wa Bayern, Pep Guardiola, ambae alikuwa Kocha wa Barca, amesema: “Njia pekee tunaweza kufika Fainali ni kucheza vyema kupita Barca. Tutajaribu hadi mwisho!”
Hata hivyo, Mabingwa hao wa Germany wanakabiliwa na kazi ngumu mno kwa vile sasa wapo kwenye wimbi baya mno la kufungwa Mechi 4 mfululizo huku Barca wakiwa wanaelea kwenye ushindi wa Mechi 8 mfululizo huku 7 zikiwa bila kufungwa hata Goli.
Kibaya zaidi ni kuwa Bayern watatinga Mechi hii bila ya Mastaa wao Majeruhi Franck Ribery, Arjen Robben, Holger Badstuber na David Alaba wakati Barca haitakosa hata Mchezaji mmoja.
Katika Mechi za Ligi za kwao Wikiendi hii iliyopita, kila Timu ilipumzisha Wachezaji kadhaa wakipiga jicho Mechi hii yao ya Jumanne.
Guardiola aliwapumzisha Wachezaji Wanne wa Timu ya Kwanza walipofungwa 1-0 na Augsburg ambao ni Kipa Manuel Neuer, Kiungo Xabi Alonso na Mabeki Mehdi Benatia na Rafinha.
Barca wao walipumzisha Wachezaji Watano lakini wakaifunga Real Sociedad 2-0 na hao ni pamoja na Andres Iniesta, Jordi Alba na Sergio Busquets.
Akiongelea Mechii, Straika wa Barca, Robert Lewandowski amesema: "Lazima tujitume kwa kila kitu. Mara nyingi tumeonyesha uwezo wetu hapa Munich. Bado vita haijaisha na tutapigana hadi mwisho!"
Lakini Barcelona, ambao wanawania ushindi wao wa 48 katika Mashindano yote Msimu huu ambayo itakuwa Rekodi kwa Klabu yao, wanatambua kibarua kigumu kinachowakabili na Beki wao Marc Bartra amesema nia yao ni kutanga Fainali.
Ameeleza: “Tunajua si kazi rahisi. Tuliona nini kiliwatokea Porto hapa hivyo lazima tutue Uwanjani kuikabili Mechi kubwa!”
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA:
Mechi za Marudiano
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumanne Mei 12
Bayern Munich v FC Barcelona [0-3]
Jumatano Mei 13
Real Madrid CF v Juventus FC [1-2]
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni