LOGO

RATIBA/MATOKEO:
Jmapili Machi 8
Mgambo JKT 3 Ndanda FC 1
Mtibwa Suga v Mbeya City
Simba 1 Yanga 0
MCHEZAJI MGANDA alieleta vuta nikuvute kati ya Klabu Vigogo Nchini baada ya kuhama kwenda nyingine kwa mizengwe mikubwa, Emmanuel Okwi, Leo hii alileta raha kubwa kwa Simba baada ya kufunga Bao pekee na la ushindi walipoilaza Yanga Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi  Kuu Vodacom.
Bao hilo la Okwi lilifungwa Dakika ya 53 na kuipandisha Simba hadi Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 17 na juu yao wapo Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 30 kwa Mechi 16 na Yanga bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 31 kwa Mechi 16.
Yanga walimaliza Mechi hii wakibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu karibuni na mwisho.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top