LOGO

 Evans and Papiss Cisse clash near the half-way line at St James' Park following the unpleasant exchange
BEKI wa Manchester United Jonny Evans na Fowadi wa Newcastle Papiss Cisse wameshushiwa Vifungo vikali kwa Kosa la kumeana mate wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Jumatano iliyopita Uwanjani St James Park ambayo Man United walishinda 1-0.
Cisse, ambae alikiri Kosa lake, amefungiwa Mechi 6 pamoja na moja ya ziada kwa vile Msimu huu tayari alishawahi kuwa Kifungoni wakati Evans, aliekanusha Shitaka lake, amefungiwa Mechi 6.
Tukio hilo, ambalo halikuonwa na Refa, lilitokea Dakika ya 38 ya Gemu hiyo ambapo Evans alimvaa Cisse alieanguka chini na Evans kuonekana akitema mate upande wa Cisse ambae baada ya kuinuka alimtemea mate Evans shingoni.
Kabla ya FA kutangaza kufungua Mashitaka dhidi yao, Papiss Cisse alimwomba radhi Jonny Evans pamoja na Wadau wa Soka lakini, Evans alikanusha kukusudia kumtemea mate Cisse na kudai si hulka yake kufanya kitendo cha aina hiyo.
FA, Chama cha Soka cha England, kimedai Kosa hilo ni kinyume na Sheria yao E1[a].

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top