.jpg)
YANGA SC imeanza vizuri michuano ya
kombe la Shirikisho barani Afrika kufuatia kuichapa mabao 2-0 BDF XI ya
Botswana katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali uliomalizika jioni hii
uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Mabingwa hao mara 24 wa Tanzania
walianza mechi hiyo kwa kuonesha kandanda safi na katika dakika ya kwanza ya
mchezo waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Mrundi, Amissi Tambwe aliyefunga
kwa kichwa akimalizia mpira wa kona wa winga machachari, Simon Msuva.
Tambwe aliyekuwa na umakini leo alitia
kambani bao la pili dakika ya 55’ kwa njia ya kichwa akimalizia krosi ya Mrisho
Khalfan Ngassa.
Katika vipindi vyote viwili, Yanga
walitawala mchezo wakicheza pasi nyingi, lakini walishindwa kutengeneza nafasi
nyingi za kufun
Hata hivyo Yanga waliendelea kupoteza
baadhi ya nafasi walizopata na wangekuwa makini wangepata ushindi mkubwa zaidi.
Kikubwa walichofanikiwa BDF XI ni
kucheza mpira wa kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza.
Malengo yao yalikuwa kukwepa kichapo
kikubwa ili wakajipange upya nyumbani na ndio utamaduni wa michuano mikubwa
barani Afrika.
Kitu wanachotakiwa kujirekebisha Yanga
ni kucheza mpira wa pasi wenye madhara, kwasababu wanajikuta wakigongeana pasio
nyingi katika eneo lao na kushindwa kuisogeza timu na kulazimisha mashambulizi.
Mechi ya nyumbani lazima utumie mbinu
nyingi kufika langoni kwa mpinzani hata kama anacheza soka la kujihami zaidi.
Yanga wanastahili pongezi kwa ushindi
huo waliopata kwasababu BDF wanahitaji ushindi wa mabao 3-0 ili kuwatupa nje
Yanga.
Kwa upande wa Yanga wanahitaji kufungwa
bao 1-0 au sare ya 1-1 ili kusonga mbele na kwa uwezo waliokuwa nao
Wanajangwani wanaweza kushinda.
Kikubwa ni kuongeza nidhamu hasa katika
kutumia nafasi wanazopata na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Baada ya Yanga, kesho uwanja wa Azam
Complex, Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc watachuana na
mabingwa wa Sudan, EL Merreick katika mechi ya raundi ya kwanza ligi ya
mabingwa barani Afrika.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni