YANGA Leo wamechukua rasmi uongozi wa Ligi Kuu Vodacom baada ya Nahodha wao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufunga Bao moja na pekee huko Mkwakwani, Tanga walipoilalisha Coastal Union Bao 1-0.
Bao hilo lilipatikana katika Dakika ya 12 kufuatia Mpira wa Kurushwa wa Mbuyu Twite kuparazwa kwa Kichwa na Mchezaji kutoka Liberia Kpah Sherman na Cannavaro kuumalizia kwa Kichwa.
Ushindi huu umewaweka Yanga Nambari Moja kwenye Msimamo wa Ligi wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC na kisha Mtibwa Sugar.
Ligi itaebdelea tena Jumamosi lakini Yanga wapo dimbani Jumapili kuivaa Mtobwa Sugar Jijini Dar es Salaam.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni