
Azam FC, mabingwa
watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara wamefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo
wa ligi hiyo baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 5-2 kwenye Uwanja wa Azam
uliopo Chamazi, Mbande jijini hapa jioni hii.
Mabao mawili ya kiungo Frank Domayo na
washambuliaji Kipre Tchetche na Didier Kavambagu, aliyefunga moja, yamewapa
uongozi wa ligi hiyo Azam FC wakifikisha pointi 25 sawa na Yanga SC waliowafunga
Mtibwa Sugar FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumapili na kukaa
kileleni kwa muda, lakini wanalambalamba wanabebwa na tofauti nzuri ya mabao ya
kufunga na kufungwa.
Mechi hiyo ya kipigo kikubwa kwa Mtibwa
Sugar FC msimu huu na kipigo kikubwa zaidi cha ligi hiyo msimu huu,
imeshuhudiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij aliyekuwa Jukwaa
Kuu la Uwanja wa Azam.
Kagera Sugar FC, timu ndugu na Mtibwa
Suga FC, ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC kwenye uwanja huo huo msimu
uliopita, kikiwa ni kipigo kikubwa kwa tmabingwa hao wa Kombe la Tusker 2008
katika miongo miwili iliyopita.
Timu hiyo inayomilikiwa na familia ya
tajiri mkubwa nchini, Said Salum Bakhresa (SSB), imefunga mabao 22 na kufungwa
12 wakati Yanga SC wamefunga mabao 15 na kuruhusu nyavu zao kutikishwa mara
saba. Timu zote mbili zimecheza mechi 13.
Dakika ya 19 tu ya mchezo, mshambuliaji
Tchetche, anayetoka kwa mabaingwa wa Afrika mwaka huu, Ivory Coast, alifunga
mlango wa mabao kwa wenyeji Azam FC akiuwahi mpira uliogonga mwamba kutokana na
shuti la winga mpya na hatari Brianm Majwega.
Hilo lilikuwa bao la pili kwa Tchetche
katika mechi mbili baada ya kufunga pia bao la kwanza katika sare yao ya 2-2
dhidi ya Polisi Moro mjini Morogoro Jumamosi.
Kwa bao hilo, Tchetche, mfungaji bora
wa ligi kuu ya Bara msimu wa 2012/13 na mchezaji bora wa ligi hiyo msimu
uliopita, akafikisha mabao matano ligi kuu ya Bara msimu huu sawa na Ame Ally
Amour wa Mtibwa Sugar FC na Danny Mrwanda wa Yanga SC.
Dakika nne kabla ya nusu saa ya mchezo,
kiungo Domayo aliyerejea uwanjani Januari baada ya kukaa nje kwa muda mrefu
kutokana kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini mwaka jana, alipatia
bao la pili Azam FC akimalizia pasi fupi ya winga 'fundi' Majwega iliyopenyezwa
ndani ya boski.
Hilo ni bao la pili kwa Domayo baada ya
kufunga pia bao pekee katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu akiwa na kikosi
cha Mcameroon Jopseph Omog waliyoshinda 1-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja
wa CCM Kambarge mjini Shinyanga Januari 17.
Domayo alikuwa na nafasi ya kufunga bao
katika shambulizi kali la kwanza la Azam FC, lakini akapaisha. Ilikuwa mechi ya
tatu ya ligi kuu kwa Domayo ndani ya kikosi cha Azam FC.
Katika dakika ya 34 Musa Nampaka
alifumua shuti la kushtukiza na kuwapatia Mtibwa Sugar FC bao akiitendea haki
pasi murua ya Mzanzibar Ally Shomari Sharrif. Hilo ni bao la kwanza kwa Nampaka
msimu huu.
Kinara wa mabao Didier Kavumbagu
alihakikisha anaendelea kuiwakimbia Samwel Kamuntu wa JKT Ruvu Stars na Rashid
Mandawa wa Kagera Sugar FC wenye mabao sita baada ya kuifungia Azam FC bao la
tatu baada ya kupewa pasi safi na kiungo Salum Abobakar 'Sure Boy' dakika tano
kabla ya mapumziko.
Kwa bao hilo, Mrundi huyo amefikisha
mabao nane msimu huu ambayo ni sawa na mabao yote aliyoyafunga mfungaji bora wa
ligi hiyo msimu uliopita, Mrundi mwenzake Amisi Tambwe katika raundi saba za
awali msimu uliopita.
Tchetche amerejea tena kambani dakika
ya nne kabla ya kipenga cha mwisho na kufikisha mabao sita ligi kuu msimu huu
akiwakamata Mandawa, Ame na Kamuntu. Tchetche amemalizia krosi nzuri
iliyomiminwa na beki wa pembeni Shomari Kapombe baada ya gonga gonga nyingi
zilizofanywa na kikosi cha Azam kuanzia katikati ya uwanja.
Dakika mbili kabla ya saa ya mchezo,
Domayo aliyejiunga na Azam FC muda mfupi baada ya kumalizika kwa msimu uliopita
akitokea Yanga SC, alitupia bao la nne kwa timu yake, la pili kwake katika
mechi ya leo na la tatu kwake msimu huu baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na
kipa Mohamed kutokana na shambulizi kali la wanalambalamba.
Dakika 12 baada ya goli hilo, yaani
katika dakika ya 70, Ame Ally Amour alifunga bao la pili kwa Mtibwa Sugar FC
akimalizia kwa ufundi pasi maridhawa ya mtokeabenchini Abdallah Juma ambaye
ulikuwa mpira wake wa kwanza tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya
mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan 'Mgosi'.
Vikosi vilikuwa;
Azam FC: Manula, Kapombe, Nyoni/ Bocco
(dk.65), Moradi, Wawa, Bolou/ Mudathir Yahya (dk. 55), Tchetche, Domayo,
Kavumbagu/ Mcha (dk.80), Sure Boy na Majwega.
Mtibwa Sugar SC: Said Mohamed, Andrew
Vicent, Majaliwa Mbaga, Ally Lundenga/ Vicent Barnabas (dk. 46), Salim Mbonde,
Shaban Nditi, Ramadhani Kichuya, Musa Nampaka, Ame Ally Amour, Henry Joseph/
Ally Shomari (dk.33) na Musa Hassan 'Mgosi'/ Abdallah Juma (dk. 70).
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni