Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam kucheza na timu ya Mgambo JKT kutoka mkoani Tanga katika
muendelezo wa michezo ya VPL mzunguko wa nane.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio
Maximo amesema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo wa siku
ya jumamosi dhidi ya Mgambo JKT na kurudi katika nafasi mbili za juu za msimamo
wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Maximo amesema tumecheza vizuri
mechi tatu zilizopita, matokeo ya mechi dhidi ya Kagera Sugar hatukugemea
kupoteza mchezo, lakini naamini katika Uwanja wa Taifa tuna nafasi nzuri ya
kupata ushindi na kucheza kandanda safi.
Aidha Maximo amesema wachezaji wote
wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mgambo JKT kesho, nawaheshimu wapinzanii
wetu ni wazuri kwa sababu hii ni Ligi na kila mmoja anahitaji pointi tatu
muhimu tumejiandaa kupata ushindi.
"Nina kikosi kizuri chenye
ushindani, kwanza tumeshinda Ngao ya Jamii, pili tunategemea kuchukua Ubingwa
wa Ligi Kuu ya Vodacom na kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la
washindi barani Afrika mwakani" amesema Maximo.
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya
Mgambo JKT, Kikosi cha Young Africans kimeingia kambini jana jioni katika
hoteli ya Valley View kujiandaa na mchezo huo ambapo wa wachezaji wawili
Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro" na mshambuliaji Hussein Javu
wataukosa mchezo huo.
Kocha Marcio Maximo amewaomba
wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans kujitokeza kesho kwa wingi
Uwanja wa Taifa kuja kuwapa hamasa vijana na kuwashangilia katika mchezo huo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni